Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limefanikiwa kukamata
mali na vielelezo mbalimbali ikiwemo lita 780 za mafuta ya Disel, vifaa tiba
vya Hospitali pamoja na waganga wa jadi wakiwa na vifaa vinavyotumika katika
kupiga ramli chonganishi.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, Kamanda wa
jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa Polisi Janeth Magomi
amesema katika kipindi cha mwezi mmoja kuanzia Februari 5,2023 hadi Februari
27,2023 jeshi hilo limefanya misako na doria katika maeneo mbalimbali ya Mkoa
wa Shinyanga.
Kamanda Magomi amesema jumla ya waganga watatu wa jadi
wamekamatwa wakiwa na vifaa vinavyotumika katika kupiga ramli chonganishi
ambayo hupelekea mauaji ya kikatili huku akitaja mali na vielelezo mbalimbali
vilivyokamatwa.
“Tumekamata
jumla ya lita 780 za mafuta aina ya Disel katika maeneo tofauti ya mradi wa
Reli ya mwendokasi SGR, Tumekamata waganga watatu wa jadi wakiwa na vifaa
vinavyotumika katika kupiga ramli chonganishi ambayo hupelekea mauaji ya
kikatili kama vile mauaji ya kutumia mapanga, tumekamata vifaa tiba vya
Hospitali vya aina mbalimbali ambavyo haviruhusiwi kumilikiwa na mtu pasipo na
idhini ya serikali, tumekamata pikipiki tatu zilizokuwa zinatumika katika
uhalifu ikiwemo kubeba mafuta ya wizi katika mradi wa Reli yay a mwendokasi ya
SGR”.amesema Kamanda Magomi
“Vitu
vingine tulivyokamata na pamoja na milango tisa(9) ya chuma, mabomba matatu, ya
chuma, bomba moja la alama za barabarani, tumekamata milango mitano (5) ya mbao
mzani wa kupima uzito, mashine ya kutobolea miamba, Godoro moja vitu 4 vya plastick,
ngoma moja ya shule na magitaa mawili”.amesema Kamanda Magomi
Kamanda Magomi ameeleza kuwa katika kipindi hicho
jeshi hilo limefanikiwa kukamata bangi kete 31, mashine mbili za kuchezea
kamali, Sub woofer mbili, feni moja, mtungi mmoja wa gesi pamoja na kuokoa
pikipiki mbili.
Aidha Kamanda Magomi amefafanua jumla ya kesi 16
zilizopata mafanikio kwenye Mahakama ikiwemo kesi nane (8) za makossa ya wizi
ambazo zilihukumiwa kati ya kifungo cha
Miezi mitatu hadi Miaka mitatu (3).
“Kesi
nne za wazazi kutowapeleka watoto shule ambao wao walihukumiwa kulipa faini ya
shilingi laki moja kila mmoja, kesi moja ya kujihusisha na vitendo vya ushirikiana
ilihusisha kwenda jela miezi 6, kesi moja ya kutotii amri halali ya serikali
ilihukumiwa kulipa faini ya shilingi laki moja na kesi moja ya kuingia kwa
jinai ililipwa faini ya shilingi laki mbili lakini pia kesi moja ya kupatikana
na mali idhaniwayo ya wizi ilihukumiwa kulipa faini ya shilingi laki tatu”.amesema
Kamanda Magomi
Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna
wa Polisi Janeth Magomi ametumia nafasi hiyo kuwapongeza wakazi wa Mkoa wa
Shinyanga kwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo ili kuzuia uhalifu na
wahalifu.
Kamanda Magomi amewaomba wananchi wa Mkoa wa Shinyanga
kuendelea kulipa ushirikiano jeshi la Polisi ili kutokomeza uhalifu huku
akiwataka kuacha mara moja baadhi ya askari wanaovujisha siri na wengine
kushirikiana na wahalifu na kusababisha kudhoofika kwa upatikanaji wa taarifa
za kihalifu kutoka kwa wananchi ambapo amesema hatua kali za kinidhamu
zitachukuliwa dhidi yao.
No comments:
Post a Comment